Institutional Support

Chawima Office Inaguration

Training Services

training

Wholesale of Credit

Eligibility Requirements/Masharti ya kuomba Mkopo Mfuko wa SELF

The Institution wishing to enter into a collaborative arrangement with SELF MF should fulfil the following requirements:-

1.Must be a legal entity with a valid certificate of registration. In this regard submission of a copy of certificate of registration, Business license, MEMARTS, BRELLA filing annual returns and tax clearance certificate becomes of paramount importance.

 2. Should have knowledgeable Board of Directors/Trustee. In this case submission of CV of each Board of Director / Trustee is of paramount importance.

3. Companies registered as limited by shares, should submit shareholders share certificates.

4. Should have qualified staff in the field of micro finance delivery services, and have institutional framework necessary in managing the credit program. Provide CVs of the key management personnel.

5.Should have identifiable offices with working equipment. Required to provide physical address of the location of business premises.

6.Should have a good track record of performing micro finance for at least a year, hence applying Best Practices of micro finance. Such performance needs to be supported by most recent Institution’s Audited Financial Report.

7.Should submit a credit policy approved by Board of Directors/ Trustees.

 8.Institutions will be required to pledge securities for credit facility from SELF MF. The details will be discussed with officers during loan appraisal.

9.Should submit a business plan covering a period of three years. The plan should indicate funding sources and reflect required SELF MF funding.

10.Should submit Environmental and Social Management compliance clearance form.

11.Should submit a letter of consent from the Board of the Directors/Trustees that authorizes management to borrow.

 12.If an Institution is having a loan with another lender, should submit statement of the loan balance.

 MASHARTI YA KUTOA MIKOPO KWA VYAMA VYA KUWEKA AKIBA NA KUKOPA

Kupata Mkopo kutoka MFUKO wa SELF, asasi inayoomba haina budi kutimiza masharti yafuatayo:-
  1.  Iwe imesajiliwa Kisheria na katika kuthibitisha hilo, nakala ya Hati ya kuandikishwa, Katiba na Sera ya ukopeshaji ya Asasi husika vinapaswa kuwasilishwa SELF. Kwa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo sera iwe imeidhinishwa na mkutano mkuu wa wanachama.

  2. Iwe na ofisi ya kudumu inayotambulika iliyo na vitendea kazi. (Eleza bayana anwani ya mahaliilipo Asasi (Physical address).
  3. Iwe na Bodi ya Wakurugenzi yenye uwezo wa kusimamia shughuli za Asasi husika, katika kuthibitisha hilo Asasi inapaswa kuwasilisha nyaraka zinazoonyesha sifa na wasifu wa wajumbe wa bodi/wadhamini.

  4. Iwe na watumishi wenye taaluma ya kuendesha na kusimamia vizuri utoaji wa huduma ya mikopo (Kuweka na kukopa). Katika kuthibitisha hilo Asasi inapaswa kuwasilisha nyaraka zinazoonyesha sifa na wasifu wa watumishi hao

  5. Iwe na uzoefu wa kutoa mikopo usiopungua mwaka mmoja, pamoja na rekodi nzuri ya utendaji hasa usimamizi mzuri wa mikopo. Katika kuthibitisha hilo,Asasi inapaswa kuwasilisha SELF ripoti ya ukaguzi wa mahesabu iliyoandaliwa na mkaguzi wa hesabu specifically (COASCO) au aliyeruhusiwa na anayetambulika na Mrajisi wa vyama vya Ushirika. (Ripoti ya ukaguzi ya karibuni – current Audit Report)

  6. Iwasilishe mpango wa biashara (Business Plan) unaonesha vyanzo vya mapato vya Asasi husika na mahitaji ya fedha kutoka SELF.

  7. Asasi husika itahitajika kutoa dhamana ya mkopo. Asasi itajadiliana na afisa wa SELF juu ya dhamana inayotakiwa, wakati wa kufanya tathimini ya mkopo.

  8. Vyama vya Akiba na Mikopo viwasilishe hati ya ukomo wa madeni iliyopitishwa na Mrajisi / au Mrajis Msaidizi wa Ushirika.

  9. Iwasilishe barua ya ridhaa ya kukopa. Kwa vyama vya Akiba na mikopo, katika kuthibitisha hilo, kumbukumbu za kikao cha mkutano mkuu (au kikao cha bodi endapo mkutano mkuu umeshapita) wa wanachama ulioridhia uongozi kukopa mkopo, zinahitajika.

  10. Kama Asasi ina mkopo mwingine toka Bank au Asasi nyingine za kukopesha inatakiwa kuwasilisha “bank statement” ya mkopo huo.

 

Maombi ya mkopo (tafadhali jaza fomu ya maombi ya mkopo) yaambatanishwe na hati husika au nyaraka (documents)  zilizotajwa kwa kadri vipengele vinavyoeleza na kutumwa kwa:

Mkurugenzi wa Mfuko wa SELF,

Barabara Mpya ya Bagamoyo - Kijitonyama,

Jengo la Letsya, ghorafa ya tatu, Kitalu Na.59 C,

S. L. P: 77760 – Dar es Salaam – Tanzania,

Simu: +255 22 2700113; Nukushi: +255 22 2700117,

Tovuti: www.self.or.tz, Barua Pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. .

Pia tumia address hizo kwa mawasiliano Zaidi.